Mahakama \ Mahakama ya Wilaya
1.0 Mamlaka ya Mahakama
- Kutekeleza mamlaka yake ndani ya Wilaya ilimoanzishwa.
- Kusikiliza mashauri ya uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji, jinai, madai, mirathi, ndoa na talaka, kuasili mtoto aliye ndugu, rufaa, mapitio, marejeo na kufanya uchunguzi wa awali wa mashauri ya jinai yanayosikilizwa na Mahakama Kuu.
- Kusikiliza madai yasiyozidi Shs. 200,000,000/=.
- Kusikiliza madai ya kibiashara yasiyozidi Sh. 30,000,000/=
- Kusikiliza shauri la mirathi lisilozidi Sh. 100,000,000/=
- Haina mamlaka ya awali katika shauri la mirathi endapo sheria inayotumika ni ya kiislam au kimila.