Courts \ High Court
1.0 Utangulizi
- Mahakama Kuu imeanzishwa chini ya ibara ya 108(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
- Mahakama Kuu inajumuisha Makao Makuu ya Mahakama Kuu Dar es Salaam, Kanda 14 na Divisheni 4 za Ardhi, Biashara , Kazi na Uhujumu Uchumi na Rushwa.
- Kanda za Mahakama Kuu ni:
- Arusha. (inayohudumia pia mkoa wa Manyara),
- Bukoba.
- Dar es Salam (inayohudumia pia Mikoa ya Pwani na Morogoro).
- Dodoma (inayohudumia pia Mkoa wa Singida).
- Iringa (inayohudumia pia Mkoa wa Njombe).
- Mbeya.
- Moshi.
- Mtwara (inayohudumia pia Mkoa wa Lindi).
- Mwanza (inayohudumia pia Mikoa ya Geita na Mara).
- Songea.
- Sumbawanga (inayohudumia pia Mkoa wa Katavi).
- Tabora (inayohudumia pia Mkoa ya Kigoma).
- Shinyanga (inayohudumia pia Mkoa wa Simiyu)na Tanga.
2.0 Malengo
Kutoa haki kwa wakati.
3.0 Majukumu ya Mahakama Kuu
- Kusikiliza na kutolea maamuzi ya migogoro yote ya madai na jinai;
- Kusisimamia Mahakama za chini;
- Kusikiliza rufaa kutoka katika Mahakama za Hakimu Mkazi, Mahakama za wilaya na mabaraza;
- Kutoa maamuzi maombi ya mapitio ya maamuzi ya kiutawala;
- Kusikiliza na kutolea maamuzi mashauri ya kikatiba.
4.0 Uongozi katika Mahakama Kuu
Shughuli za utendaji wa kila siku wa Mahakama Kuu na Mahakama za chini zinasimamiwa na Jaji Kiongozi. Katika kutekeleza majukumu yake anafanya kazi za kusimamia uendeshaji wa mashauri na za utawala. Madaraka ya Jaji Kiongozi ya usimamizi wa mashauri katika ngazi ya Mahakama Kuu Kanda na Divisheni yamekasimiwa kwa Majaji Wafawidhi . Na katika ngazi ya Mahakama za Hakimu Mkazi, Wilaya na Mwanzo madaraka hayo yamekasimiwa kwa Mahakimu Wafawidhi . Shughuli za utawala zinafanywa na Wasajili na Watendaji wa Mahakama.
5.0 Mamlaka ya Mahakama Kuu katika usikilizaji wa mashauri
5.1 Mashauri ya Jinai
- Mashauri ya mauaji, ugaidi nay a uhujumu uchumi ambayo hayana kibali cha DPP kusikilizawa na Mahakama za chini.
- Rufaa toka mahakama za Hakimu Mkazi na Wilaya.
5.2 Mashauri ya Madai
- Mashauri ya ndoa, mirathi, biashara na ardhi yenye dhamani ya shilingi 300 milioni kwa mali inayohamishika na shilingi 200 milioni kwa mali isiyohamishika.
- Rufaa toka Mahakama za Hakimu Mkazi na Wilaya.
- Rufaa toka Mahakama Kuu hupelekwa katika Mahakama ya Rufani.