Courts \ Court of Appeal
1.0 Utangulizi
- Mahakama ya Rufani ilianzishwa tarehe 15 Agosti, 1979 baada ya kufa kwa iliyokuwa Mahakama ya Afrika Mashariki. Mahakama hii imeanzishwa kwa mujibu wa ibara ya 117(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
- Mahakama ya Rufani ina mamlaka Tanzania bara na Zanzibar.
- Kimsingi ndiyo Mahakama ya mwisho katika utoaji wa haki nchini.
- Mahakama hii haina mamlaka ya awali (Original jurisdiction) isipokuwa ina mamlaka ya kusikiliza na kutoa maamuzi ya rufaa, maombi ya mapitio , marejeo na masahihisho.
- Rufaa na maombi yanayowasilishwa Mahakama ya Rufani ni kutoka katika Mahakama Kuu Tanzania bara, Mahakama Kuu Zanzibar na kutoka kwenye mabaraza maalumu kama vile Baraza la Rufaa za Kodi.
2.0 Dira
Dira ya Mahakama ya Rufani ni ile ya Mahakama ya Tanzania: Haki sawa kwa wote na kwa wakati. Mahakama ya Rufani inalenga kutoa huduma bora kwa ustadi na weledi wa hali ya juu.
3.0 Uongozi katika Mahakama ya Rufani
- Mhe. Jaji Mkuu ndiye Kiongozi Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Mahakama ya Rufani. Kwa sasa Jaji Mkuu ni Mhe. Jaji Prof Ibrahim H. Juma. Jaji Mkuu wa Kwanza mzalendo alikuwa ni Jaji Augustino Said(marehemu). Waliofuatia na Jaji Francis Lucas Nyalali (marehemu), Jaji Barnabas Albert Samatta, Jaji Augustino S.L. Ramadhani na Jaji Othman Chande.
- Ifuatayo ni orodha ya Majaji ambao waliwahi kushika wadhifa wa Jaji Mkuu tangu kuanza kwa Mahakama ya Tanzania:-
- Mheshimiwa William Morris Carter C.B.E. - 1920 - 1924
- Mheshimiwa William Alison Russel 1924 - 1929
- Mhe. Joseph Alfred Sheridan - 1929 - 1934
- Mhe. Sidney Solomon Abrahams - 1934 - 1936
- Mhe. Llewelyn Chisholm Dalton - 1936 - 1939
- Mhe. Ambrose Henry Webb - 1939 - 1945
- Mhe. George Graham Paul - 1945 - 1951
- Mhe. Herbert Charles Fahie Cox - 1952 - 1955
- Mhe. Edward John Davies - 1956 - 1960
- Mhe. Ralph Windham - 1961 - 1964
- Mhe. Jaji P. Telford Georges - 1965 - 1970
- Jaji Augustino Said - 1971 - 1977
- Jaji Francis Lucas Nyalali - 1977 - 2000
- Jaji Barnabas Albert Samatta - 2000 - 2007
- Jaji Augustino S.L. Ramadhani - 2007 - 2011
- Jaji Mohamed Chande Othman - 2011 - 2017
- Pof. Jaji Ibrahim H. Juma - 2017 –
• Kiutawala, Jaji Mkuu anasaidiwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Msajili Mkuu wa Mahakama. • Chini ya Msajili Mkuu kuna Msajili wa Mahakama ya Rufani ambaye pamoja na manaibu wakw huratibu na kusimamia shughuli za kila siku za kimahakama.
Majukumu ya Mahakama ya Rufani
- Jukumu kuu la Mahakama ya Rufani ni kusimamia suala la utoaji haki nchini. Katika kutekeleza jukumu hili, Mahakama ya Rufani hutafsiri sheria mbalimbali kwa kusikiliza na kutokea uamuzi mashauri yote yanayowasilishwa mbele yake. Maamuzi haya hutoa msimamo wa sheria katika jambo lililoamuliwa msimamo ambao unapaswa kufuatwa na mahakama zote za chini.
Uendeshaji wa mashauri kwa njia ya vikao.
- Kwa asilimia kubwa mashauri yanayofunguliewa Mahakama ya Rufani husikilizwa kwa njia ya vikao (Court Session).
- Katika usikilizaji wa Mashauri Mahakama inaundwa na jopo la Majaji watatu, watano au saba. Vilevile kuna maombi ambayo husikilizwa na Jaji mmoja. Yapo pia Mashauri ambayo husikilizwa na Jaji mmoja hasa yale ya maombi ya kuongezewa muda.
- Vikao vya Mahakama ya Rufani hupangwa kupitia kalenda ya mwaka wa kisheria yaani kuanzia mwezi February kila mwaka. Hufanyika katika kanda zote za Mahakama ya Rufani ambazo kwa sasa ni kumi na mbili . Kanda hizo ni:
- Arusha.
- Bukoba.
- Dar es Salaam.
- Dodoma.
- Iringa.
- Mbeya.
- Mwanza.
- Mtwara.
- Tabora.
- Sumbawanga.
- Tanga.
- Zanzibar.
- Pale ambapo kunakuwepo na maamuzi kinzani baina ya majopo, Mhe. Jaji Mkuu huunda jopo la Majaji watano (full bench of the Court) ili kutoa msimamo sahihi wa Mahakama. Pia kuna masuala kama vile ya kikatiba ambayo humpelekea Mhe. Jaji Mkuu kuunda jopo lenye Majaji tano au saba (full bench of the Court).
- Maamuzi ya Mahakama ya Rufani ni ya mwisho na ni muongozo unaopaswa kufuatwa na vyombo vyote vya utoaji haki Nchini.